“Sitachukua hata Dola moja kwenye mshahara wa Urais”,
ni kauli ya Rais mteule Donald Trump baada ya kuulizwa kwamba atakuwa
akiufanyia nini mshahara wa Dola laki nne (400,000 kwa mwaka) ambazo ni
mshahara wa Rais wa Marekani anapokuwa Ikulu ya White House.
Kauli hii aliitoa Donald Trump mshindi wa
kiti cha Urais nchini Marekani wakati akiwa kwenye kampeni zake
September 17, 2015, huko Rochester, New Hampshire: “Kitu cha
kwanza ninachotaka kuwaambia na nitakifanya kama nikichaguliwa kuwa
Rais, Sitakuwa nikichukua mshahara, hata dola moja siihitaji, hicho sio
kitu kikubwa kwangu.” – Donald Trump
Kwa mujibu ripoti mpya zilizotolewa na
jarida la watu maarufu duniani Forbes, limetaja utajiri wa Rais huyo
mteule kuwa unafikia Dola Bilioni 3.7 za Marekani ambazo ni zaidi ya
shilingi Trilioni 8 za Tanzania
Katika Video hapa chini, Donald Trump
anasikika akisema kwamba alikuwa akijigharamia kwa fedha yake mwenyewe
wakati wa kampeni zake, hivyo hatachukua mshahara wake zaidi ya kupokea
vitu vidogo ambavyo ni vya lazima akiwa Rais.
VIDEO: Rais mteule Donald Trump akizungumzia kutohitaji mshahara wa Urais akiingia Ikulu ya White House
0 comments:
Post a Comment