Familia ya “Rais Mteule” wa Marekani
Donald Trump inazidi kuzimiliki headlines kubwa wakati ikijiaandaa
kuingia Ikulu ya White House. Mbali na nafasi aliyoipata mfanyabiashara
huyo tajiri, Trump anaishi maisha ya kifahari kwenye jumba lake lenye
thamani ya shilingi za Tanzania zaidi ya Bilioni 215.
Jumba hilo liko kwenye eneo lenye ukubwa
futi za mraba elfu themanini (80,000) ufukweni mwa jiji la Florida.
Trump alinunua jumba hilo kwa dola za Marekani Milioni 5 mwaka 1985 na
kulifanyia ukarabati ambapo sasa lina vyumba vya kulala 58, bafu 33,
jiko lenye meza za Marble kwa ukubwa wa futi 29, pamoja na sehemu za
kuwasha moto 12.
0 comments:
Post a Comment