Mwanadada kutoka Nigeria, Yemi Alade akizikonga nyoyo za mashabiki waliohudhuria tamasha la Fiesta 2016 Imoooo katika Viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam leo Novemba 5, 2016.
Mwanamuziki kutoka Nigeria, Tekno Miles akilishambulia jukwaa la Fiesta 2016.
Mashabiki wakifuatilia shoo ya Fiesta 2016 ndani ya Viwanja vya Leaders Club usiku huu.
Tekno na vijana wake wakifanya yao.
Ali Kiba “King Kiba” akiwapa raha mashabiki wake waliofurika katika Viwanja vya Leaders Club kwa ajili ya Fiesta 2016.
King Kiba akiimba sambamba na King of the best melodies, Christian Bella.
King Kiba akizidi kuwapa raha mashabiki.
Baraka Da Prince akikatika sambamba na madansa wakati akiimba wimbo aliomshirikisha Ali Kiba.
Abby Skillz akiimba jukwaani wimbo aliomshirikisha Kiba.
Mwana Hip hop, Roma Mkatoliki akishusha mistari juu ya jukwaa la Fiesta 2016.
Roma Mkatoliki na Stamina wakiwa stejini na mavazi yao ya mabondia.
Chid Benz akifanya yake.
Mr Blue akiwapagawisha mashabiki waliofurika katika hitimisho la msimu wa Fiesta 2016.
Mwanamuziki Chegge Chigunda na madansa wake wakionyesha umahiri wao stejini.
Baadhi ya wafanyakazi wa Clouds Media ambao ni waandaaji wa Fiesta wakiwa stejini.
Mwanamuziki Ben Pol akiwaburudisha mashabiki.
Mwana RnB, Ben Pol akiwapa raha mashabiki.
Mashabiki wakiwa wakolea na burudani za Fiesta 2016.
Burudani zikiendelea.
Mtangazaji wa Clouds FM, Adam Mchomvu akisema na mashabiki.
Dogo Janja akikisanua stejini.
Mzee wa Too Much, Darasa akiwapa shangwe wapenda burudani.
Mwanamuziki TID a.k.a Mnyama a.ka. Kigoo akifanya yake kwa steji.
King of the best melodies, Christian Bella akiwapa raha Wana Dar es Salaam.
Mwanamuziki Raymond “Rayvan” kutoka WCB akilishambulia jukwaa la Fiesta 2016 Imooo.
Nyomi ikifuatilia shangwe za Fiesta 2016 Imooo.
Vijana wakionyesha umahiri wao wa kucheza ‘karate’.
Hatimaye ile shoo kubwa iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na wapenzi wa burudani jijini Dar es Salaam ili kuhitimisha msimu wa Fiesta 2016 imefanyika leo Novemba 5, 2016 ndani ya Viwanja vya Leaders Club na kuhudhuriwa na maelfu ya wakazi wa jiji hilo.
Shoo hiyo imeongozwa na wasanii kutoka nje ya nchi wakiwemo Tekno Miles “Tekno” na Yemi Alade wote kutoka Nigeria pamoja na Dk. Jose Chameleone kutoka nchini Uganda.
Wasanii wa hapa waliozikonga nyoyo za mashabiki wa burudani ni pamoja na Alikiba “King Kiba”, Weusi, Juma Nature, Mr Blue, Darasa, Christian Bella “King of the best melodies”, J Mo, Jux, Shilole, Snura, Raymond “Rayvan”, Baraka Da Prince, Vanessa Mdee, TID, Roma Mkatoliki, Stamina, Fid Q, Ommy Dimpoz, Abby Skillz, Dogo Janja, Billnas, Young D, Belle 9, Barnaba na wengineo.
0 comments:
Post a Comment