The blog is about hard news



Tuesday, November 15, 2016

Fuata Njia Hizi, Mwanamke Hakukatai Ng`oo Hata Awe Vipi


Kifupi unakuta mwanaume ana status nzuri tu lakini anakosa mwanamke anayejielewa.yaani wengine hadi wananiuliza sometimes mimi "hivi wewe unawapataje wanawake wazuri na wanaojimbua hivo".

Sasa leo nimeona ni vyema nikishare na nyinyi namna ya kumnasa demu hata awe ni anajitambua vipi!

1: Unapoomba namba ya simu hakikisha huombi kwa papara, yaani usioneshe kama una shida sana na usioneshe kama unataka kumtongoza, bali onesha kama unataka tu ulafiki wa kawaida,yaani lafiki wa kuchati nae tu kawaida.

2: Akikupa namba leo kausha usimtafute leo leo, mtafute baada hata ya wiki,msalimie tu na umpigie, hapa uangalie na muda ambao unadhani mtu anakuwa free, sio kupiga simu asubuhi sana au mchana au usiku sana, piga mida ya saa mbili usiku,na usiongee nae zaidi ya dakika 5.

3: Hakikisha kila siku unamtumia msg mara 3 na kumpigia simu mara moja, yaani asbh mtakie asbh njema, mchana, jioni na usiku piga kumpa pole na heka heka za mchana, ongea nae si zaidi ya dakika 5 ili usimchoshe.

4: Hakikisha hutumii maneno ya mtaani sana mfabo oya,inakuwaje,michongo vipi, barida, mzuka, poa n.k. Tumia maneno mazuri ya busara mfano sawa, haya, umeshindaje, habari yako, n.k. yaani asikuone wewe hujitambui.

5: Weka nae urafiki wa kudumu kiasi kwamba awe anakumiss, na ukimtext asipojibu mtumie vocha hata ya buku. Ila angalia usitumie pesa sana.

6: Omba outing nae, na akikubali basi mpeleke sehemu tulivu yenye adabu na sio mnaenda bar, mkiwa huko ongelea zaidi maisha ya kawaida ya mwanadamu, usiongelee ishu za X wako kamwe, ishu za mapenzi usiongelee kabisa, weka vistory vya kuchekesha ili awe anafurahi na kukumiss mkitoka hapo.

7: Ukiwa unapiga nae stori kwenye simu usiwe unaongea sana, na hata mkiwa pamoja basi usiongee sana kama chiriku, pangilia maneno sana ya kuongea(waza kabla ya kusema).

Baada ya urafiki wa kama miezi miwili hivi, hapo sasa mtamkie wazi wazi kwamba unampenda tangu muda mrefu, na umtongoze kwa heshima sana. Nakuhakikishia hapo hachomoki hata kwa dawa.

NB: Mbinu hizi ni za kuwapata tu wanawake wanaojielewa, wanaotaka mwanaume/mpenzi na sio wanaotaka pesa. Kwa wale wanawake vicheche, we tumia pesa tu, ukimtongoza leo jioni basi kesho unamfunua
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Copyright © JARIDALETU BLOG | Powered by Blogger