Wakati Durant alikuja juu na kuwa superstar, Thabeet hakuwahi kuweza kufikia hatua hiyo, akiwa ametokea chuo cha Connecticut, na kucheza katika timu nne za NBA na tatu za D-League kabla ya kuwa mchezaji ambaye yuko huru kucheza timu yeyote nab ado hajachukuliwa na timu yeyote mpaka mwaka 2015.
Durant bado anamatumaini makubwa na Hasheem na kwamba ipo siku atapewa nafasi.
Kwa maneno yake alisema: ‘Hasheem anajua hamna mtu anayemuonea huruma, na wala yeye mwenyewe hajionei huruma, yeye ni ni mmoja wa wachezaji wenye juhudi na pia ni mtu mzuri sana, na ni mmoja kati ya mchezaji mwenza mzuri sana kuwahi kuwa nao karibu. Ipo siku atapata nafasi, kwa sasa anajaribu kuwa mvumilivu’.
Baada ya kuumia kwa hisia zake aliposhindwa kuendelea NBA, Thabeet mwenye umri wa miaka 29 sasa, anaamini kwamba, mwili wake, akili yake na uwezo wake kimchezo umeshapikwa na kuiva sasa baada ya kuenda San Francisco kufanya mazoezi na Frank Matrisciano na Meneja wa zamani wa NBA, Milt Newton mwishoni mwa mwezi Aprili.
Thabeet aliongelea kujifunza kwake mpira wa kikapu tangu akiwa na miaka 15 hapa nchini Tanzania mpaka kufikia kuchaguliwa kuwa Na. 2 kwenye draft ya NBA na mpaka baadae kufeli kabisa.
Kwa sasa Hasheem anaamini bado umri wake unaruhusu, alipokua kiakili mwkaa jana ni tofauti na alipole hii, mazoezi anayofanya mniji San Francisco yamemsaidia sana kutengeneza mwili na kuchonga kiakili, ana imani sana na mwalimu wake wa mazoezi.
Ameamua kubakia nchini Marekani kuendelea na mpira huo wa kikapu. Anajua wazi Watanzia tunamuangalia na tunamuamini sana.
Alipoulizwa ni kitu gani ambacho angeweza kufanya tofauti katika kipindi chote alichochezea Ligi ya NBA, alisema angeendelea kuwa mtulivu kama livyokuwa na kufanya kile tu alichopswa kufanya. Na cha zaidi angeliomba kuuliza au kuambiwa sababu kwanini hawakuendelea naye tena. Kwani kitendo cha kumuengua mtu bila kusema wapi amekosea, hakumjengi mchezaji.
0 comments:
Post a Comment