The blog is about hard news



Friday, November 18, 2016

Haya Hapa Matokeo ya Forbes Person of the Year Aliyokuwa Anawania Rais Magufuli


Aliyekuwa Mwendesha Mashtaka wa Serikali na Wakili nchini Afrika Kusini Thuli Madonsela leo ametangazwa kuwa ndiye mshindi  wa Tuzo ya Mtu Mashuhuri Afrika ya Forbes (Person of the Year #POY2016).

Tuzo huyo hupewa mtu aliyetoa mchango mkubwa katika kuiinua jamii kwenye njanja mbalimbali za maisha kama vile uchumi, siasa, utamaduni.

Katika kinyang’anyiro cha tuzo hiyo, Thuli Madonsela alikuwa akichuana na Michiel Le Roux kutoka Afrika Kusini, Rais wa Mauritania, Ameenah Gurib, Jamii ya watu wa Rwanda na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.

Mwaka 2015 tuzo hii ilikwenda kwa Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya MeTL, Mohammed Dewji.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Copyright © JARIDALETU BLOG | Powered by Blogger