The blog is about hard news



Monday, November 21, 2016

Kajala: Sijawahi Kuwa na Mahusiano ya Kimapenzi na Paul Makonda


Msanii wa filamu za kibongo, Kajala Masanja amevunja ukimya na kufunguka kuhusu maneno yaliyokuwa yanazunguka mwa muda mrefu mitaani yakimtaja kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa nyakati tofauti na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda tangu akiwa DC wa kinondoni alipokuwa akishirikiana kwa karibu na msanii huyo kwenye shindano la kusaka vipaji vya wasanii wa Wilaya ya Kinondoni lililojulikana kama Kinondoni Star Search.

Katika mahojiano na mwandishi wa habari hizi, Kajala alipoulizwa kuhusu madai ya kuwa na uhusiano na Makonda, alijibu kwa haraka na kwa kifupi: “Hapana sijawahi kutoka naye kabisa. Hilo halipo.”

RC Makonda aliwahi kuzungumzia madai hayo akiwa bado Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, ambapo alisema ni propaganda zinazoelezwa na wabaya wake wa kisiasa ambao wamekuwa wakisaka mbinu za kumchafua kila kukicha.

“Ni muda mrefu tu, walianza kipindi kile wakati wa Bunge la Katiba nilipokwenda Bungeni na mwigizaji Yobnesh Yusuf ‘Batuli’, wakasema natembea naye, wakanyamaza. Sasa wamehamia kwa Kajala baada ya kufanya naye kazi", alisema Makonda.

“Hakuna ukweli wowote wanatungatunga tu mambo, watakuwa na sababu zao kwa sababu mtu kama Kajala, maneno yameibuka baada ya kufanya naye project ya kutafuta vipaji vya wasanii.“

"Nimeshirikiana na wasanii wengi wa kiume katika project hiyo lakini kwa kuwa wameona mwanamke ni Kajala peke yake, wanasema vitu ambavyo havina kichwa wala miguu. Najua kuna wengine wanaoeneza haya mambo wanatumika kisiasa lakini mimi sijali".
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Copyright © JARIDALETU BLOG | Powered by Blogger