Idadi ya watu waliojitokeza mahakamani katika kesi ya Lema leo imekuwa ndogo sana ukilinganisha na uhamasishaji uliofanyika.
Picha zinazorushwa kutoka maeneo ya mahakama hazioneshi zile “nyomi” tulizozizoea pindi Lema anapopelekwa mahakamani.
Hata wanachama kindakindaki wanaofuatilia kesi hii kwenye mitandao kama Facebook wamekuwa wakimtaja Bananga pekee kama chanzo cha taarifa kutoka mahakamani.
Hata tukio linalopewa umaarufu la mwanamke anayedaiwa kuzimia linaripotiwa kwa picha inayoonesha watu wachache sana wakiwa na mama huyo.
Muda umefika Lema atathmini siasa zake zisije zikampa maumivu makali kuliko matokeo yaliyotarajiwa.
0 comments:
Post a Comment