The blog is about hard news



Wednesday, November 30, 2016

NISHA Akanusha Kupewa Mimba na Nay wa Mitego


Baada ya msanii wa filamu Salma Jabu, Nisha kulalamika kubakwa na kupewa mimba na msanii wa muziki na baadaye kudai msanii huyo ameikataa mimba hiyo. Mashabiki katika mitandao ya kijamii walidhani mimba hiyo ni ya Nay wa Mitego hali ambayo ilimfanya rapa huyo kukanusha uvumi huo.


Rapa huyo kupitia kipindi cha U head cha Clouds FM amekanusha kumpachika mimba mrembo huyo huku akidai hajaonana naye kwa kipindi cha miaka 3.

“Mimi sielemi nimeshirikishwaje kwenye suala la mimba, tena naambiwa nimembaka, hivi mimi ninavyogombaniwa na wanawake naanzaje kumbaka?,” alisema Nay wa Mitego.

Baada ya kauli hiyo, muigizaji huyo wa filamu za vichekesho ameweka mambo sawa kupitia Instagram yake kwa kusema kuwa hakuwai kusema kuwa ana mimba ya mpenzi wake huyo wa zamani, Nay wa Mitego.

“Naywamitego iko hivi kabla hujaandika kitu chunguza sio unakurupuka tu na kuandika ujinga. Ulinisikia na kuniona wapi nimekutaja kwamba wewe ndo baby dady wangu???? hivi naanzaje kuzaa na wewe Nay?? kifupi pamoja na mapungufu na makosa yaliyojitokeza kwa baba k wangu humfikii hata kwa kucha labda umemshinda hizo tatoo zako kama bibi harusi. Nikuombe msamaha kwa kipi acha kudandia treni kwa mbele.??? tena watishe hao hao WANAUME SURUALI mimi simuogopi yeyote anayekojoa akiwa amesimama wala amechutama,” aliandika Nisha
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Copyright © JARIDALETU BLOG | Powered by Blogger