The blog is about hard news



Wednesday, November 30, 2016

PESA Aliyoitoa Ronaldo kwa Familia za Wachezaji Waliofia Katika Ajali ya Ndege



Bado dunia na ulimwengu wa soka kwa sasa unaomboleza msiba wa msafara wa timu yaChapocoense ya Brazil uliyopata ajali wakati wakielekea kutua uwanja wa ndege waMedellin Colombia.

Ajali hiyo ya ndege imehusisha watu 81 kati ya hao 76 wamepoteza maisha huku 72 kati ya hao walikuwa ni sehemu ya msafara wa timu hiyo na wachezaji wakielekea kucheza mchezo wao wa fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Atletico Nacional ya Colombia.

Cristiano Ronaldo ni mmoja kati ya mastaa wa soka walioguswa kwa kiasi kikubwa na msiba huu, Ronaldo ameamua kuchangia euro milioni 3 ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 9.6 kwa timu yaChipacoense na familia za wachezaji wa timu hiyo waliyopoteza maisha.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Copyright © JARIDALETU BLOG | Powered by Blogger