Anaandika Comred Mbunge wa Jimbo la Tarime vijini John Heche.
Mahakama za Tanzania ni aibu kwa taifa, mahakama inapokua sehemu ya kunyima haki inafundisha watu tabia ya kutoheshimu mahakama.
Hili sakata la Lema kuna mtu aliniambia mapama litapigwa danadana mpaka feb kwa visingizio mbalimbali mwanzo sikuamin!
Sasa imethibitika hivyo inatia hasira sana. Kesi yenye dhamana inawezekana vipi kunyimwa dhamana!
Kama kesi ya kuota mtukufu amekufa haina dhamana ni bora ikaunganishwa na zile tatu za mauaji,uhaini na armed robbery ambazo sheria zetu zinatambua kwamba hazina dhamana, vinginevyo ni mahakama kutumika vibaya kunyima watu haki zao, na watu wataendelea kuona maona hata kama mtukufu hayapendi.
#Justice for Lema.
0 comments:
Post a Comment