Muimbaji huyo ameliambia gazeti la Mtanzania kuwa baada ya kushindwa kufanya vizuri kwenye nyimbo za ujumbe ndio akaangalia ni kitu gani mashabiki wanataka akaamua kubadilika.
“Mwanzo nilikuwa nikitoa nyimbo zenye vionjo vyenye ujumbe wa kutosha lakini hazikuwa zikipokelewa sana ila nilipokaa na kufikiria zaidi, nikatambua nini mashabiki wanataka na ndiyo maana muziki wangu upo juu sana tofauti na zamani,” amesema.
Rapper huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wa ‘Muziki’ uliogeuka kama wimbo wa taifa kwa sasa.
0 comments:
Post a Comment