The blog is about hard news



Monday, December 5, 2016

Situmii Dawa za Kutunisha Misuli - Young Dee


Msanii wa hip hop nchini Paka Rapa (Young Dee) amesema hatumii dawa zozote za kukuza misuli yake na mwili wake bali anafanya mazoezi kila siku na bado hajafikia katika kiwango ambacho anataka kufikia.

Hata hivyo akiongea kupitia eNewz, Young Dee amesema anazingatia chakula, muda  wa mazoezi na muda wa kupumzika na pia anazingatia sana chakula  chenye protini na mahali pazuri pa kulala, hizo ndizo sababu ambazo zinampelekea kuwa na mwili mkubwa kwa sasa.

Pia Yong Dee amemalizia kwa kusema kwamba hajawahi kuachana na mpenzi wake Tunda hivyo hata sasa Tunda anavyomposti katika mitandao yake na kumshukuru Young Dee ni kutokana na ushauri ambao alimpa hivi karibuni kuhusiana na maisha yake.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Copyright © JARIDALETU BLOG | Powered by Blogger