The blog is about hard news



Thursday, December 1, 2016

Ziara ya Uingereza ya Diamond na Ne-Yo yasogezwa mbele



Kama ulijipanga kufuatilia ziara ya Diamond na Ne-Yo ya nchini Uingereza mwezi Disemba mwaka huu basi jipange upya. Ziara hiyo imesogezwa mbele.

Kwa sasa ziara hiyo itaanza Machi 29 na kufikia mwisho April 8 ya mwakani. Awali ziara hiyo ilitarajiwa kuanza Jumatano ya Disemba 7 kwenye ukumbi wa Clasgow Barrowland na kufikia mwisho Disemba 14 ya mwaka huu.

Kupitia mtandao wa Instagram, Ne-Yo ameandika, “The December dates have been postponed! But don’t worry U.K. I’m still headed your way with NEW DATES and my bro @diamondplatnumz. 2017, let’s turn up! Tickets available at RoboMagicLive.com #NEYOUKLive.”

Naye meneja wa Diamond, Sallam kupitia mtandao huo ameandika, “UK New Dates…!! @neyo and @diamondplatnumz 😎.”
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Copyright © JARIDALETU BLOG | Powered by Blogger