Sio kitu cha ajabu kusikia wasanii wakiwarusha wanamichezo kwenye ngoma zao. Hiki kitu kimeanza muda mrefu sana ndani ya Africa hadi nje ya Africa. Mmoja kati ya wanamichezao waliohi kutajwa sana kwenye nyimbo za HipHop huko marekani ni Michael Jordan au M.J kama wanavyomuita.
Tumeongea na Diamond Platinumz ambapo yeye na wasanii wake wa WCB wamekua wakitaja majina ya wana michezo mara kadhaa kwenye ngoma zao hasa Ronaldo na Mbwana Samatta.
Diamond tulipomuuliza kuna faida gani kwake na kipi kinamvutia kutaja majina ya wachezaji hao kwenye ngoma zake. Jibu lilikua hili “Hata kama mtu anafanya kazi kiasi gani kama jamii haijamkubali basi bado ana kazi ya ziada ya kufanya hadi akubalike.”
Aliendelea “Sasa mimi nawataja watu ambao wamefanikiwa kukubalika na jamii, ukiangalia watu kama Ronaldo na Samatta inaongeza chachu ya nyimbo na kupendwa zaidi. Hata wao pia wanafarijika kuona kwamba sisi kwa sisi pia tunakubaliana kwa kila kitu tunachofanya.”
0 comments:
Post a Comment