Ben Pol ameiambia Bongo5 kuwa kinachoonekana ndicho kilichofanyika – walikuwa na muda mzuri kiasi cha kumfanya akiri kuwa hajawahi kufurahia kufanya video kama ilivyokuwa kwenye hiyo.
“Ni video ambayo nimefanya bila kuchoka. Kwasababu kwanza tulikuwa tunahave fun wamekuja akina Jux pale. Wale warembo pia waliwekuwepo, watu wako charming, wako very happ yaani,” anasema muimbaji huyo.
“Hata walinzi waliokuwepo pale pembeni walikuwa kama wanatutamani fulani, yaani tulikuwa kama tunahave fun kiukweli.”
Ben pia anasema aligundua kuwa Darassa ni mtu anayependwa na ni rahisi mtu yeyote kumzoea. “Naweza kusema Darassa ni mtu rahisi kufanya naye kazi.”
0 comments:
Post a Comment