The blog is about hard news



Saturday, November 26, 2016

Ali Kiba atolea ufafanuzi picha za nyumba zilizowekwa mitandao ikidaiwa ni nyumba yake

Mwanamuziki Ali Kiba amejitokeza hadharani na kusema kuwa yeye bado anaishi kwenye nyumba ya kupanga na kuwa picha za nyumba zilizosambazwa mitandaoni si nyumba yake kama ilivyodaiwa.
Ali Kiba aliyasema hayo jana alipokuwa akifanya mahojiano na kituo kimoja cha redio cha jijini Dra es Salaam ambapo alisema kuwa picha zilizosambazwa kwenye mitandao ya jamii kipindi cha nyuma si za nyumba yake, na kuwa yeye anaishi kwenye nyumba ya kupanga.
Siku za hivi karibuni ziliwekwa picha na video kwenye mitandao ambapo Ali Kiba alionekana katika nyumba hiyo huku watu wakisema kuwa nyumba ni ya msanii huyo. Picha hizo zilionyesha maeneo kama mbalimbali ya nyumba hizo kama jikoni kukiwa kumenakshiwa vizuri.
Baada ya muda mfupi wa picha hizo kusambazwa, ilikuja kuelezwa kuwa haikuwa nyumba ya Ali Kiba kama ilivyodaiwa na kuwa ni duka la samani za ndani ambapo Ali Kiba alikuwa dukani hapo, na ni ndugu yake ndiye aliyechukua video na kupiga picha kisha kuanza kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii. 
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Copyright © JARIDALETU BLOG | Powered by Blogger