Tuzo za mwaka huu za All Africa Music Awards 2016 zinatarajiwa kufanyika Jumapili hii kwenye ukumbi uliopo kwenye hoteli ya Eko ya jijini Lagos Nigeria.
Nimekuwepo huku Nigeria kuanzia Ijumaa hii na maandalizi yake ni kuvutia. Kabla ya tuzo zenyewe leo, kumekuwepo na matukio ya utangulizi ikiwemo show ya Afrima Music Village siku ya Ijumaa. Jumamosi, wageni ambao wengi wao ni wasanii waliotajwa kuwania tuzo hizo kutoka nchini mbalimbali za Afrika, walizungushwa katika mji wa Lagos kufahamu maeneo muhimu katika mji huu.
Miongoni mwa sehemu waliyopewa maelezo ya kihistoria ni katika eneo lililotumiwa na wakoloni, Freedom Park. Tazama picha Zaidi.
0 comments:
Post a Comment