welding
Mapenzi au uhusiano na kazi ni vitu viwili vinavyoendana sana. Linapokuja suala la kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mtu, wakati mwingine si jambo linalotokea tu, bali kazi watu wanazozifanya huchagia pia.
Uchunguzi uliofanywa na mtandao wa Bloomberg Business wa nchini Marekani umebaini kuwa kazi mtu anayoifanya inaweza kukuonyesha kuwa ni mtu wa aina gani utakaye muoa au kuolewa naye.
Hii hapa chini ni orodha ya kazi na mtu unayeweza kumuoa au kuolewa naye kama unafanya kazi hiyo.
Mwalimu Shule ya Msingi au Sekondari
Mwalimu wa kike katika shule ya msingi au sekondari ana nafasi kubwa ya kuolewa na mwalimu wa kiume anayefanya kazi hiyo hiyo. Hii si lazima wawe wanafundisha shule moja. Kwa upande wa mwalimu wa kiume, atakuwa na anfasi  kubwa ya kumuoa mwalimu wa kike.
Sekta ya Fedha
Mfanyakazi wa kike katika sekta ya fedha ana nafasi kubwa ya kuolewa na meneja au mkuu wa kitengo anachofanyia kazi au kutoka taasisi nyingine inayojishughulisha na masuala ya fedha, wakati mwanaume kwenye sekta ya fedha anauwezekano mkubwa wa kumuoa mwalimu.
Mhudumu wa ndege
Mhudumu wa kike anakuwa na uwezekano mkubwa wa kuolewa na meneja au mkuu wake wa kitengo wakati mhudumu wa kiume anakuwa na nafasi kubwa ya kumuoa mwalimu.
Mtaalamu wa mapishi
Mpishi wa kike ana nafasi kubwa ya kuolewa na mkuu wa kitengo cha mapishi, mpishi mkuu au mpishi mwingine wa kiume. Kwa upande wa mpishi mwanaume kuna uwezekano akamuoa mhudumu wa mgahawa/baa au mpishi mwenzake wa kike.
Afisa biashara
Afisa biashara wa kike huenda akaolewa na mtumishi mwezake katika idara hiyo huku afisa biashara wa kiume anaweza akamuoa afisa biashara wa kike au muuguzi.
Mkulima na msimamizi wa ranchi za mifugo
Kwa upande wa mwanamke anayefanya kazi, anaweza kumuoa mwanamume anayefanya kazi kama hii, muuguzi katika hospitali wakati mwanaume anaweza kumuoa mwanamke mkulima au mwalimu.
Daktari
Daktari mwanamke anauwezekano mkubwa wa kuolewa na daktari wa kiume wakati kwa upande wa daktari wa kiume anaweza kumuoa daktari wa kike, muuguzi, au mwalimu.
Mhudumu katika mgahawa/hoteli/baa 
Mhumudumu wa kike ana uwezekano mkubwa wa kuolewa na mpishi katika eneo lake la kazi au mhasibu wakati mhudumu wa kiume anaweza kumuoa mhudumu wa kike, mpishi au mfanya usafi.
Mwigizaji
Mwanamke muigazaji anauwezekano mkubwa wa kuolewa na muigizaji wa kume au mwanume yeyote anayejishulisha na sanaa mfano, msanii, mtayarisha muziki au filamu wakati mwigizaji wa kiume yeye huenda mwigizaji wa kike, mwanamke anayefanya sanaa au mwanasheria.
Wanasheria na Majaji
Wanasheria au majaji wanawake wao ni rahisi kuolewa na wanasheria au majaji wa kiume na hivyo hivyo kwa upande wa wanaume.
Wakurugenzi (CEOs)
Uchunguzi umeonyesha kuwa Wakurugenzi wanawake wana nafasi kubwa ya kuolewa na wakurugenzi wa kiume wakati wakarugenzi wa kume wana nafasi kubwa ya kuoa walimu.
Wafanyakazi wa ndani
Wafanyakazi wa ndani wa kike wana nafasi kubwa ya kuolewa na walinzi wa nyumba, wafanyakazi wanaotunza bustani au wamchinga lakini wafanyakazi wa ndani wa kiume kuna uwezekano mkubwa wa kuoa wafanyakazi wa ndani au wahudumu wa mgahawa.
Madereva wa malori
Madereva wa malori wa kike mara nyingi huolewa na madereva wakiume wa malori sababu hutumia muda mwingi wakati mmoja wakati madereva wa kiume huwaoa Makatibu Muhtasi (secretary) au wasaidizi wengine kwenye ofisi.
Afisa wa Polisi
Polisi wa kike ana nafasi kubwa ya kuolewa na Polisi wa kiume wakati Polisi wa kiume hupendelea kuoa walimu.
Msanii
Msanii wa kike ana nafasi kubwa ya kuolewa na msanii mwenzake wa kume na kwa upande mwingine, mwigizaji wa kuime ana nafasi ya kumuoa mwigizaji wa kike au mwalimu.
Mafundi Mwashi, Seremala
Mwanamke ambaye ni fundi mwahi au seremala mara nyingi huolewa na mafundi wa kiume wakati mafundi wa kume mara nyi huwaoa wafanyakazi wa ndani, wahudumu au wafanya usafi.
Mtu siyekuwa na kazi 
Mwanamke asiye na kazi na ambaye kwa miaka mitano iliyopita hakuwa na kazi, utafiti umeonyesha kuwa anauwezekano wa kuolewa na mwanaume anayefanya biashara ndogo ndogo, wakati kwa mwanaume anaweza kumuoa mwalimu, msaidizi wa ndani na mfanyabiashara ndogo.
Wanenguaji
Wanenguaji wa kike wanuwezekano wa kuolewa na wasanii mbalimbali, mafundi wanaochomea au wayeyisha vyuma wakati wanenguaji wa kiume wao wana uwezekano mkubwa kuwaoa wanenguaji wenzao, wasanii wa kike, wa Katibu Muhtasi.
Mtaalamu wa masuala ya akili (Psychologists)
Kwa upande wa mwanamke, ni rahisi kwake kuolewa ya mwanasaikolojia wa kiume wakati kwa mwanaume yeye, anaweza kumuoa mwanasaikolojia wa kike au mwalimu wa sekondari