The blog is about hard news



Thursday, December 29, 2016

PRODUCER Mr T Touch Adai Hataki Kusikia Habari za Nay wa Mitego


Mtayarishaji wa muziki wa bongo fleva Mr T Touch ambaye kwa mwaka 2016 ametengeneza ngoma nyingi kali na zilizofanya vizuri katika vyombo mbalimbali vya habari amefunguka na kusema haitaji tena kumzungumzia Nay wa Mitego

Mr T Touch ambaye alikuwa ni moja kati ya maproducer wa Nay wa Mitego ambaye ametengeneza ngoma nyingi za Nay wa Mitego zilizofanya vyema sana kipindi cha nyuma alisema anawashukuru sana watu ambao wamekuwa na mchango kwake katika kufanikiwa na kupiga hatua za maendeleo.

"Nilishasema zihitaji habari za kiuhanagwa kama hizi, mimi sihitaji kumzungumzia huyo Nay wa Mitego, tuzungumzie shughuli yangu na mipango yangu kwa mwaka 2017 kwani mjini usipokuwa na shughuli watu hawawezi kukuelewa kidogo, kwa hiyo tusimzungumzie atakapokuwa na shughuli nadhani hiyo shughuli itanihusu kwa hiyo tusimzungumzie" alisikika Nay wa Mitego kwenye kipindi cha eNEWZ

Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Copyright © JARIDALETU BLOG | Powered by Blogger