MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba na timu ya Taifa ya Uganda, Emmanuel Okwi amevunja mkataba wa kuichezea klabu ya Sonderjyske Fodbold ya Denmark baada ya pande zote mbili kufikia makubaliano.
Okwi amefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na uongozi wa klabu hiyo baada ya kutopata nafasi ya kutosha kuichezea tangu alipojiunga nayo mwaka 2015 akitokea Simba.
Mtandao huo ulimnukuu Mkurugenzi wa Soka wa klabu hiyo, Jorgen Haysen, akisema maamuzi hayo yamefikiwa baada ya Okwi (24), kushindwa kupata nafasi ya kucheza kwa muda mrefu.
“Okwi hajapata muda wa kutosha kucheza kwenye timu yetu, na hata matarajio ya kupata muda zaidi wa kucheza hayajaongezeka.
Hivyo basi tumekubaliana kuuvunja mkataba huu. Tunamtakia kila la heri," alisema Haysen kwenye taarifa ya mtandao huo maarufu wa michezo.
Okwi alisaini mkataba wa miaka mitano na alitegemewa angekuwapo kwenye kikosi hicho mpaka mwaka 2020.
Nyota huyo pia amewahi kuzichezea klabu za SC Villa ya Uganda , Etoile de Sahel ya Tunisia na Yanga.
Kwa muda mrefu tangu kuanza kwa msimu huu wa Ligi Kuu mara kwa mara Okwi amehusishwa kutaka kurejea kwenye kikosi cha Simba japo viongozi wa timu wamekuwa wakikanusha taarifa hizo.
0 comments:
Post a Comment