WAKATI baadhi ya mabinti wanaohusika kama video queens kutajwa katika sakata la madawa ya kulevya hivi karibuni, Gift Stanford ‘Gigy Money’ ameibuka na kusema baadhi yao wanaponzwa na kuiga aina ya maisha anayoishi, hivyo kujikuta wakijihusisha na ishu hiyo.
“Naona wanapenda kuniiga maisha yangu sana, sijawahi kubeba au kutumia unga na sina hofu kabisa ya kutajwa maana huwa nafanya kazi halali, hao video queen wanaoiga na kutaka kuwa juu kama mimi hawajui kwamba siri ya mafanikio yangu ni kufanya kazi,” alisema msanii huyo ambaye licha ya kuwa video queen, pia ni mtangazaji wa redio.
Katika vita alivyoanzisha vya kupambana na madawa ya kulevya, Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda alitaja majina ya watu mbalimbali wanaotuhumiwa kujihusisha nayo, wakiwemo video queens, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ na Tunda Sebastian ambao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu na kuachiwa kwa dhamana.
0 comments:
Post a Comment