The blog is about hard news



Friday, February 10, 2017

Kamanda Sirro Asema Manji na Gwajima Bado Wapo Lupango, Aeleza Walioripoti Leo ..!!


Kamanda Sirro amesema  bado wanamshikilia mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji pamoja Askofu wa kanisa la Ufunuo na Uzima, Josephat Gwajima kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya kulevya.

Watuhumiwa hao wawili waliripoti kituoni hapo jana mchana na siyo leo kama walivyoagizwa na RC Paul Makonda. 

Kamanda Sirro amesema atatoa taarifa Jumatatu kueleza nini kinaendelea kuhusu watuhumiwa hao. 

Mpaka wakati anazungumza na waandishi wa habari kamanda huyo alisema walioripoti kituoni hapo ni watuhumiwa 4 kati ya 65 . 

Walioshuhudiwa na waandishi wa habari wakiripoti kituoni hapo ni Iddi Azzan, Hussain Pamba Kali pamoja na bosi Sea Cliff.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Copyright © JARIDALETU BLOG | Powered by Blogger