The blog is about hard news



Wednesday, November 9, 2016

Donald Trump achaguliwa kuwa Rais mpya wa Marekani

Donald Trump amechaguliwa kuwa Rais mpya wa Marekani baada ya kumshinda mpinzani wake, Hillary Clinton. Tayari Clinton amempigia simu na kukubali kushindwa.
3a32924000000578-3918258-image-a-32_1478678489019
Donald ameshinda majimbo ya uchaguzi 276, huku Clinton akishinda 218.
Kushindwa kwa Clinton kumekuwa pigo kubwa zaidi katika maisha yake ya kisiasa hasa kwakuwa wengi walimtabiria ushindi na kuwa rais wa kwanza mwanamke. Akihutubia baada ya kutangazwa mshindi, Trump amempongeza Clinton na kusema amefanya kazi kubwa na kwa muda mrefu na kwamba anastahili kulipwa fadhila.
Amewaomba Wamarekani hata wale ambao hawakumpigia kura, kumuunga mkono kwenye safari yake ya kulijenga taifa hilo.
3a3295e700000578-3918258-thanks_trump_went_through_his_family_naming_his_wife_and_each_of-a-1_1478678895161
“For those who have chosen not to support me in the past – of which there were a few people – I am reaching out to you for your guidance and your help so that we can unify our great country,” alisema.
“As I have said from the beginning, ours is not a campaign but a great movement, made up of millions of hard-working men and women. No dream is too big. No challenge is too great. Nothing we want for our future is beyond our reach. America will no longer settle for less than the best,” aliongeza.
Trump anakuwa rais wa 45 wa Marekan
Share:

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Copyright © JARIDALETU BLOG | Powered by Blogger